Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

MADAKTARI BINGWA WA RAIS SAMIA WAPUNGUZA GHARAMAZA MATIBABU KWA WANANCHI ZAIDI YA 650 KIGOMA.

Posted on: May 6th, 2024



Na WAF, Kigoma

Kambi ya Madaktari bingwa wa Dkt. Samia mkoani Kigoma imewapunguzia gharama za kufuata huduma za kibingwa na ubingwa bobezi kwa wananchi zaidi ya 650 kupitia huduma ya mkoba ya madaktari bingwa wa Rais Samia

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa wilaya ya Kigoma Mhe. Salum Kali mara baada ya uzinduzi wa huduma ya mkoba ya madaktari bingwa wa Rais Samia katika hospitali ya rufaa ya Mkoa Mawezi, Kigoma.

Mhe. Salum amesema kuwa wananchi hao wamepatiwa huduma kutoka kwa Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni siku ya kwanza ya utoaji huduma katika kambi ya matibabu ya kibingwa inayofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni-Kigoma huku kambi hiyo ikionekana kuwa na tija kwa wananchi kwani imepunguza gharama za kufuata huduma za kibingwa nje ya mkoa wao.

Hata hivyo Mhe. Kali amewataka madaktari hao kutoa huduma na kuainishi magonjwa yanayowasumbua wananchi ili kujua jinsi ya kuongeza huduma kulingana na uhitaji.

Kwa upande wake daktari bingwa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi Dkt. Serafini Patrice amesema kuwa awali walikuwa wanafanya kambi moja moja kwa kila hospitali katika kanda ya Magharibi lakini kwa sasa wanafanya kwa kushirikiana kama timu katika hospitali za kanda ya magharibi.